Monday, October 4, 2010

Mrehemu AMINA CHIFUPA
Mungu alailaze roho yake mahali pema paponi  AMIN........
lakini mtoto alikuwa na ......................Mhhhhhhhhhhhhh
  Mipango ya Mungu haikwepeki lakini tulitamani angekuwepo Amina atukumbushe enzi zake za leo tena kipindi hicho ikianza saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana.Tunamkumbuka japo hayuko nasi bado anaendelea kuishi na sisi mioyoni mwetu kwa kumbukumbu nzuri alizotuachia.Nakumbuka siku za mwisho kabla mwenyezi hajamchukua alikuwa kila siku ananiomba nimpigie wimbo wa Lady Jaydee siku hazigandi na rail on ya papa wemba.
We miss you....R.I.P Amina Chifupa.

Geah Habib,mimi,Zamaradi katika super friday...super leo tena.

Dian na kipindi chake chake LEO TENA na 88.4 Redio ya watoto wa mjini
 Nimefanya kazi kwa miaka 4 sasa sijawahi kuchukua likizo,ila safari hii nimeamua kupumzika nikasalimie ndugu jamaa na marafiki.Namuacha Gea Habib atakaimu nafasi yangu na atakupa kitu roho inapenda.Tuombeane heri nikirudi tuendelee kuwa pamoja tena katika leo tena.

 Ml Criss kipindi hicho anafanya Dr.Beat kabla ya kuitwa Xxl...kwa sasa yupo choice fm(102.6 fm) radio nyingine chini ya clouds entertainment...

Filamu mpya ya REY
PRETTY GIRL

baadhi ya wajumbe ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisubili kuupokea mwenge ulioanza mbio zake mkoani Kagera wakati ukitokea mkoani Mwanza.Picha na Audax Mutiganzi.

mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu

kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Henry salewi akipokea mwenge toka kwa mkimbiza mwenge kitaifa Dr. Nassoro Ali Matunzya.

Gari aina ya Subaru lenye namba za usajiri T 193 AZL ikiwa katika hali mbaya sana mara baada ya kupata ajali jioni hii maeneo ya Kinondoni,Ubalozi wa Ufaransa.gari hii ambayo ilikuwa ikitokea maeneo ya Kinondoni Morocco kuelekea mjini,ilipoteza muelekeo mara baada ya gari moja kuingia ghafla katika barabara kubwa huku gari hii ikiwa katika mwendo wa kasi sana na kumfanya dereva wa gari hii kushindwa kuikontroo gari hii na kwenya kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani na kuifanya ikapinduka.ndani ya gari hii kulikuwemo na watu watatu ambao wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospital na mwingine kufanikiwa kutoka bila jeraha lolote.




OBAMA akiwa ndani ya White House USA

Rais Barack Obama wa Marekani akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wetu nchini humo Mh. Balozi Mwanaidi Maajar (katikati) pamoja na mume wake, Bw. Shariff Hassan Maajar pamoja na mjukuu wao Kai-Hassan katika Ikulu ya Marekani wakati alipokabidhi hati ya utambulisho.

JK akimnadi MO Jimbo la Singida Mjini.



MO akiwawasalimia wana Singida Mjini mara baada ya kunadiwa na JK katiika mkutano wa kampeni uliofanyika jana Jimboni humo


Wilson Elisha Khambaku akiongea kwa hisia kwenye mkutano wa kampeni Ikungi kuhusu siku 29 alizokaa Chadema baada ya kuanguka kwenye mchakato wa CCM

Wilson Elisha Khambaku akiongea na wana Ikungi katika mkutano wa kampeni.

 
====================
  • Alikaa Chadema siku 29
  • Atoa siri, Chadema hakuna sera
  • Wapinzani zaidi ya 50 warudi CCM
  • Wasanii watoa buradani ya kishindo

Aliyeshindwa kura za maoni jimbo la Singida Magharibi na kuhamia Chadema kwa siku 29, Bwana Wilson Elisha Khambaku, ameeleza kilichomsibu akiwa kwenye chama hicho pinzani.

Akitoa ushuhuda kwenye mikutano ya kampeni Puma na Ikungi, Khambaku alikiri kughafilika na kukimbilia upinzani baada ya kuanguka kwenye kura za maoni.

Akishangiliwa na umati wa watu pale aliposema kwamba aliomba sera za Chadema kwa wiki moja bila mafanikio na hatimaye kushindwa kupata muelekeo wa chama hicho kwa ajili ya kampeni.

Alisema chama hicho ni matapeli kwani baada ya kumzungusha wiki mbili walimpa sera za matusi na kubeza mafanikio thabiti ya CCM.

Akiongelea mafanikio ya CCM kwenye upanuzi wa elimu ambapo hata Umoja wa Mataifa umetambua na kuipa Tanzania tuzo ya kukidhi malengo ya milenia kwenye upande wa elimu kwa asilimia 95.

Akizungumza kwa hisia kubwa, Khambaku alisema siku 29 alizokaa Chadema zilikuwa za mateso na upweke mkubwa, akizifananisha na nyumba yenye kunguni na chawa ambazo humuwasha mtu anayelala kwenye malazi yake.

Amesema sababu kubwa zilizomfanya yeye kurudi CCM ni amani na utulivu iliyodumishwa na CCM tangu uhuru hadi leo. Amewasihi wananchi wa Singida wasifanye makosa ya kuchagua upinzani, ni wasanii, wana chuki na wanabeza hata mafanikio halali ya CCM.

"Mwisho nawasihi msifanye makosa niliyofanya mimi, msihangaike na wapinzani. Hawana sera hao, nimejionea mwenyewe! Naomba mchague chama madhubuti, CCM"

Alimaliza Khambaku huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Na kwenye mkutano wa kampeni wa Ikungi, wapinzani zaidi ya 50 kutoka Chadema na CUF walirudisha kadi zao na kuingia CCM.

Aliyehama kutoka Chadema, alitoa ushuhuda kwa kusema alipochukua kadi ya Chadema aliambiwa kwamba yeye ni mwenyekiti.

"Nikawauliza mwenyekiti wa nini, wakasema wa kijiji hiki. Nikawahoji nani kanichagua? na ninamuongoza nani? Sikupewa jibu, sasa narudi CCM" Alisema Mzee huyo akishangiliwa na umati wa watu.

Nao wasanii wa muziki hawakuwa nyuma kwenye kutoa hamasa kwenye mkutano huo. Mwanamuziki Flora Mbasha akisindikizwa na wanamuziki wengine mashuhuri Ray C na Bushoke walitoa hamasa kubwa kwa wananchi wa Ikungi waliohudhuria kwa wingi mkutano huo wa kampeni.

Naye mshairi maarufu kutokea hapa Singida alitumbuiza kwa shairi lake lililomshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kuleta wilaya mpya ili kusogeza shughuli za maendeleo karibu na wananchi.

Mshairi huyo alisifia umahiri wa Chama Cha Mapinduzi haswa kuwatayarisha viongozi wa nchi na utawala mzima wa chama. Alisema kutoka umoja wa vijana kuna jumuiya ya wazazi na wanawake ambazo zote zinalenga kuwalea wana CCM kuongoza chama na nchi. Alihoji wapinzani wanapikwa namna hiyo hadi kutaka kugombea uongozi wa juu wa nchi?

Akishangiliwa na umati wa watu, mshairi huyo alisihi pia kudumisha amani na mshikamano haswa kipindi cha uchaguzi. Aliwasihi wana Singida kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili mkoa uongoze kwenye kura nyingi kwa wagombea wote wa CCM.

Kabla ya Mkutano wa Ikungi - Singida Mashariki, Mheshimiwa Kikwete alifanya mkutano wa kampeni Puma Singida Magharibi ambapo mgombea ubunge wa jimbo hilo Mohamed Missanga alimshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kuwapatia wilaya mpya na jimbo jipya la uchaguzi.

Baada ya hapa, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Itigi, Manyoni, Kitinku na hatimaye Dodoma Mjini kwa mkutano wa mwisho wa kampeni kwa siku ya leo.

kwa habari hizi na zingine nyingi katika kampeni ya JK

MO akiwahutubia wana Singida Mjini

Wana CCM wakisikiliza mkutano

JK akiwa na MO pamoja na watoto waliokuwepo wakati wa kumpokea alipokuwa akiingia katika hospitali ya rufaa inayojengwa Singida



Wana CCM wakiwa wamelizunguka gari la JK

 
Maalim Seif akimpa kadi mwanachama mpya wa CUF

 
Picha za ufunguzi wa kampeni wa CUF

 

 
                                       Maalim Seif aitangaza ilani ya chama cha wananchi CUF 

 

 

Maalim seif akitoa hutuba baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea uraisi wa znz